MPRU NA TANAPA WAKUTANA NA KUBADILISHANA UZOEFU KATIKA ENEO LA USIMAMIZI NA MIFUMO YA UKUSANYAJI WA MAPATO
MPRU NA TANAPA WAKUTANA NA KUBADILISHANA UZOEFU KATIKA ENEO LA USIMAMIZI NA MIFUMO YA UKUSANYAJI WA MAPATO

Jumatano, Juni 11, 2025, Arusha

Wataalamu kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) wametembelea Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa lengo la kubadilisha uzoefu katika eneo la Usimamizi na Mifumo ya Ukusanyaji wa Mapato, na zaidi namna ya kuhudumia wateja pale Mifumo ya utoaji huduma inapokuwa na changamoto Tarehe 09 Juni, 2025 katika Mkoa wa Arusha.

Wataalam hao watatu (3) kutoka MPRU walioshiriki ziara hiyo walikuwa ni Mhasibu Mwandamizi, Bw. Sweetbert Frances, Afisa TEHAMA, Bw. Yusuph Rajabu pamoja na Afisa Sheria, Bw. Chaila Lupindu ambao waliongoza uwakilishi wa MPRU katika ziara hiyo.

Aidha, Wataalamu hao kutoka MPRU, walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha (Ngongongare Gate) kwaajili ya kujifunza taratibu zinazotumika katika kuhudumia wageni wanaoingia Hifadhini pamoja na taratibu zilizowekwa ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.

Halikadhalika, MPRU na TANAPA waliweza kubadilishana uzoefu na kujadili maeneo mbalimbali wanayoweza kushirikiana katika kutangaza vivutio vya utalii na kuboresha huduma kwa wateja wanaotembelea katika maeneo yao.