MPRU YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA 'KARIBU-KILI FAIR 2025'

Jumanne, Juni 10, 205, Arusha
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) imeshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ‘Karibu Kili Fair 2025' yaliyofanyika kuanzia Tarehe 06/06/2025 mpaka 08/06/2025 katika Viwanja vya Magereza, Mkoani Arusha.
Maonesho hayo yalifunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto na kueleza umuhimu wa jukwaa hilo katika kuwaunganisha watoa huduma, kutoa ajira na kunadi tamaduni zetu za asili kwa wageni washiriki.
"Kili-Fair 2025 si tu jukwaa la kutangaza vivutio vyetu, bali pia daraja la kuwaunganisha watoa huduma wa ndani na masoko ya kimataifa. Ni nafasi ya kuchochea ajira, mapato na thamani ya rasilimali zetu za kiutamaduni na kiasili”alisema Dr. Biteko.
Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibu Kili-Fair ndiyo makubwa zaidi ya utalii Afrika Mashariki, ikihusisha washiriki zaidi ya 450 kutoka zaidi ya mataifa 30.
Ushiriki katika Tamasha hilo unaipa MPRU fursa ya kuweza kutoa elimu kwa wadau wake wote watakaotembelea katika Maonesho hayo juu ya shughuli za Uhifadhi wa Bahari na ulinzi wa rasilimali zake ikiwemo Matumbawe, Mikoko na Nyasi bahari.
Lengo kuu la tamasha hilo ni kukuza utalii Tanzania na kuongeza ushirikiano wa kikanda baina ya Tanzania na Nchi za Afrika Mashariki.