MPRU YAENDESHA PROGRAMU YA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA TAASISI Y UHASIBU TNZANIA (TIA)
MPRU YAENDESHA PROGRAMU YA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA TAASISI Y UHASIBU TNZANIA (TIA)

Alhamisi, Januari 22, 2026, Dar es Salaam

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) imeendesha programu ya mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) ili kuweza kufahamu na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo kwa lengo la kuhamasisha utalii wa bahari nchini.

Mafunzo hayo yaliyofanyika Januari 22, 2026 yakiongozwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Kukuletela Lukandiga, Afisa Uhusiano, Bw. Ivan Kimaro pamoja na Afisa Habari Bw. Arafat Mnyau katika Ukumbi Mkuu wa Chuo hicho.

Wanafunzi hao walipata fursa ya kujifunza kuhusiana na Utalii wa Bahari na shughuli za Uhifadhi wa Rasilimali za Bahari zinavyoendeshwa ikiwa ni hatua moja wapo ya kuendana na sera ya Uchumi wa Buluu kuhakikisha inakua kupitia rasilimali zetu za Bahari tulizonazo nchini.