PROGRAMU YA MAFUNZO MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA SMART TANGA
PROGRAMU YA MAFUNZO MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA SMART TANGA

Jumanne, Mei 27, 2025, Tanga

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) yashiriki katika mafunzo ya kujengea uwezo kuhusu matumizi ya Teknolojia ya SMART (Spatial Monitoring and Reporting Tool), yaliyoandaliwa kwa lengo la kuimarisha mbinu za Usimamizi na Uhifadhi wa Bahari yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Nyinda Classic iliyopo katika Mkoa wa Tanga.

Mafunzo hayo ya siku tano (Mei 26-30, 2025) ambapo mpango huu wa SMART unafadhiliwa na Shirika la Wildlife Conservation Society (WCS), ambalo linaendelea kushiriki kikamilifu katika kukuza uwezo wa kitaasisi na kuimarisha Usimamizi wa rasilimali za Baharini kwa njia endelevu.

SMART ni programu ya kisasa yenye vifaa vya uchambuzi wa taarifa, iliyoundwa kusaidia juhudi za Uhifadhi kwa kuboresha ufuatiliaji wa Bayoanuwai, kuratibu doria kwa ufanisi zaidi, na kukabiliana na vitendo haramu kama vile uvuvi haramu.

Mafunzo haya yalilenga kuwajengea ujuzi watumishi wa MPRU katika ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa katika shughuli za doria, utayarishaji wa ripoti na ramani kwa ajili ya kusaidia maamuzi sahihi, ufuatiliaji wa viashiria vya utendaji, pamoja na kusawazisha mbinu za ukusanyaji wa taarifa katika maeneo tofauti ya Hifadhi.

Matumizi ya teknolojia ya SMART yanatarajia kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji katika kutekeleza ulinzi na usimamizi wa Maeneo yaliyohifadhiwa ya Bahari (MPAs).