WANAFUNZI WA TAASISI YA USTAWI WA JAMII WAPATIWA PROGRAMU YA MAFUNZO KUHUSU UTALII WA BAHARI
Ijumaa, Januari 30, 2026, Dar es Salaam

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) imeendesha programu ya mafunzo kwa wanafunzi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW) ili kuweza kufahamu na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo kwa lengo la kuhamasisha utalii wa bahari nchini.
Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Kukuletela Lukandiga kwa kushirikiana na Afisa Tehama, Bw. Abas Maige pamoja na Afisa Habari, Bw. Arafat Mnyau waliendesha program hiyo ya mfunzo kwa wanafunzi wa taasisi hiyo yaliyofanyika katika Maktaba (Library) Januari 29, 2026 jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi hao walipata fursa ya kujifunza kuhusiana na Utalii wa Bahari na shughuli za Uhifadhi wa Rasilimali za Bahari zinavyoendeshwa ikiwa ni hatua moja wapo ya kuendana na sera ya Uchumi wa Buluu kuhakikisha inakua kupitia rasilimali zetu za Bahari tulizonazo nchini.

