MIMP KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA KULINDA RASILIMALI ZA BAHARINI
MIMP KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA KULINDA RASILIMALI ZA BAHARINI

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatatu, Januari 15, 2024

Timu ya wafanyakazi kutoka Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP), VLC'S, Maafisa wa Uvuvi wa Kisiwa hicho wamebadilishana uzoefu kuhusu teknolojia ya Doria Mahiri (Smart Patrol)  ikiwa ni pamoja na matumizi ya programu ya SMART na ndege isiyo na rubani (drone)  wakati wa kufanya doria.

Teknolojia ya 'SMART PATRO'L ni njia muafaka ya kupambana na uvuvi haramu, usioripotiwa na usiodhibitiwa, kuoainisha teknolojia pamoja na mbinu za 'SMART'.

Doria husaidia kulinda Rasilimali za Bahari kwenye Hifadhi ya Kisiwa cha Mafia na kukuza matumizi endelevu ya rasilimali asilia za Bahari.

Mpango huu unafadhiliwa na World Wildlife Fund (WWF).