Muongozo wa Wageni

 

VIVUTIO VYA UTALII

  • Papa Potwe, Samaki mkubwa kuliko wote duniani
  • Magofu ya karne ya 13
  • Jamii mbili za kasa green turtle na hawksbill turtle
  • Pomboo
  • Ndege wanaohama
  • Mabaki ya sanaa za mikono ya miaka  600 .K.K
  • Bustani za Matumbawe
  • Nyangumi wanaohama jamii ya (humpback na sperm Whales)
  • Mabwawa yenye viboko na misitu mikubwa ya mikoko
  • Jamii ya kaa wakubwa duniani (coconut crabs)
  • Fukwe zenye mchanga safi na maji angavu, na fukwe ndefu zenye milima ya mchanga
  • Popo wanaokula matunda wanaopatikana maeneo ya Mafia Sychelles na Comoro tu.

SHUGHULI ZA UTALII

  • Kuogelea
  • Kuogelea na samaki mkubwa duniani (Papa Potwe)
  • Kutembelea magofu na maeneo mengine ya Kihistoria
  • Kubarizi na kulala katika fukwe za mchanga
  • Kutazama pomboo (dolphins)
  • KUogelea na kuzamia kwa kutumia vifaa maalumu (snorkelling and Diving)
  • Kutembelea katika njia vinjari (nature trails)
  • Kutazama nyangumi
  • Kuvinjari kwa kutumia boti (cruising)
  • Kuweka kambi usiku
  • Kushiriki shughuli za kitamaduni za wenyeji (vyakula,ususi n.k)
  • Uvuvi wa burudani

JINSI YA KUFIKA

HIFADHI YA BAHARI YA KISIWA CHA MAFIA

Inapatikana takribani Km 120 kusini mashariki mwa Dar es Salaam. Usafiri wa ndege hutumika kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Usafiri wa boti kwa shughuli za utalii unapatikana utende/Mafia.

MAENEO TENGEFU YA DAR ES SALAAM

kwa upande wa Visiwa vya kaskazini mwa dar es salaam boti zinapatikana Berinda/Serene,Whitesand Hotel,Magha Beach,Kibo Beach na Slipway Hotel. kwa Visiwa vilivyopo kusini usafiri unapatikana katika Hotel ya Kipepeo.

HIFADHI YA BAHARI YA SILIKANTI TANGA

Ipo mkoani Tanga na inafikika kwa boti zinapopatikana katika eneo la Yatch Club, Huku kisiwa cha Machanga cha Maziwe kilichopo km 52 kusini mwa Tanga kikifikika kwa boti zilizopo Pangani na Ushongo.

HIFADHI  YA BAHARI YA GUBA YA MNAZI

Inapatikana km 45 kutoka Mtwara mjini