UTENDAJI KAZI WA WATUMISHI WA MPRU KUPIMWA KI ELETRONIKI
UTENDAJI KAZI WA WATUMISHI WA MPRU KUPIMWA KI ELETRONIKI

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatano, Januari 31, 2024

Watumishi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) wamefanyiwa mafunzo ya mfumo wa kieletroniki wa Usimamizi wa Utendaji kazi katika Utumishi wa Umma (Public Employees Perfomance Management Information System - PEPMIS) mnamo tarehe 30 Januari 2024. Mafunzo hayo yalitolewa na serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika ukumbi MPRU Makao Makuu Upanga, Dar es Salaam.

 Mafunzo yalihusisha watumishi wa Makao Makuu pamoja na vituo vya Dar es Salaam (DMRS), Tanga (TACMP), Mafia (MIMP) na Mtwara (MBREMP). Watumishi wa MPRU Makao Makuu pamoja na DMRS walishiriki moja kwa moja huku wale wa vituo vilivyo nje ya Dar es Salaam wakishiriki kwa njia ya mtandao. Mfumo huu utasaidia kupima utendaji wa watumishi wa umma, kuboresha uwajibikaji kwa kila mtumishi na kurahisisha utekelezaji wa majukumu aliopangiwa sambamba na utoaji wa taarifa.