MAPITIO YA MPANGO WA USIMAMIZI TMRS
MAPITIO YA MPANGO WA USIMAMIZI TMRS

Tarehe Iliyochapishwa: Ijumaa, Desemba 15, 2023   

Timu ya Menejimenti ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu wameendesha kikao cha kupitia Mpango wa Usimamizi (GMP) wa Tanga Marine Reserve System (TMRS), ambao una umuhimu mkubwa unaogusa nyanja mbalimbali za mazingira, uchumi na jamii kwa ujumla.

Mpango huu unatija katika kukuza utalii pamoja na kuhimiza uwekezaji katika maeneo ya hifadhi, pia una jukumu muhimu katika kuhakikisha uhifadhi wa rasilimali kwakulinda bayoanuwai na maliasili nyinginezo, pamoja na kuendeleza ushirikiano baina ya taasisi,jamii na wadau.