MAFUNZO YA KUJENGEA UWEZO KWA MAKUNDI YA VIJANA KATIKA WILAYA YA MAFIA.
MAFUNZO YA KUJENGEA UWEZO KWA MAKUNDI YA VIJANA KATIKA WILAYA YA MAFIA.

Tarehe Iliyochapishwa: Ijumaa, June 16, 2023

WATONET (Whale Shark Tour Operators Network of Tanzania) wanatoa mafunzo ya kujengea uwezo kuhusu utalii kwa makundi ya wavulana na wasichana katika Wilaya ya Mafia.

Mafunzo hayo ni ya siku 7 ambapo yalianza toka tarehe Juni 14 hadi Juni 2023. Kwa kushirikiana na Idara ya Utalii ya Kisiwa cha Mafia (MIMP) na Hifadhi za Bahari chini ya ufadhili wa WWF (World Widelife Fund) wamelenga kuwapatia maarifa ya kujitosheleza na ujuzi kwa vijana katika kushiriki kwenye soko la Utalii na kuchochea hatua endelevu.

Idadi jumla ya vijana 30 watapata nafasi ya kujifunza kuhusu mafunzo ya biolojia na ikolojia ya Bahari chini ya wataalamu kutoka MIMP (Mafia Island Marine Park).

Ziada, Kituo cha Uzamiaji cha Mafia kitatoa mafunzo ya Huduma ya Kwanza kama sehemu ya programu.