TANGAZO LA MAFUNZO BILA MALIPO KWA NJIA YA MTANDAO

19 Mar, 2026

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Queensland kutoka nchini Australia chini ya ufadhili wa Global Environment Fund (GEF) inawakaribisha wote kushiriki katika mafunzo ya wiki tano (5) kwa njia ya mtandao bila malipo yoyote yatakayofanyika kwa saa moja hadi mbili kwa siku.

Mafunzo hayo yanalenga kuwaleta pamoja wadau mbalimbali ili kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu kati ya nchi sita (6) zinazoendesha mradi wa Global Environmental Fund (GEF) 7 – Coral Reef Rescue Initiatives (CRRI).

Bonyeza link hapo chini kuona video yenye maelezo zaidi;

https://drive.google.com/file/d/1XUzFoSUjLJARlTPVk6bnQ17vOe1PI8f6/view?usp=drive_link

https://www.instagram.com/reel/DWDruqujYyB/?igsh=b3BjcDJ1dml3OWJu