MPRU KUSHIRIKI MKUTANO WA 28 KIMATAIFA WA MABADILIKO YA TABIA NCHI (COP 28)

22 Nov, 2023

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) inatarajiwa kushiriki mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (COP 28) ulioandaliwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unaotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 30 mpaka Desemba 12, 2023 katika mji wa Expo nchini Dubai.