SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI. JUNI 5,2023.

11 May, 2023

 

Katika Siku ya Mazingira Duniani 2023,Taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu inatambua mchango mkubwa unaotolewa na serikali ya Tanzania,wafanyabiashara pamoja na wadau wengine katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira wa taka za plastiki. Juhudi hizi zinaonyesha dhamira ya pamoja ya kushughulikia suala hili muhimu na kwa pamoja tunaweza kukabiliana vilivyo na uchafuzi wa plastiki ili kulinda mifumo ya ikolojia ya baharini na kuunda mustakabali endelevu kwa wote. Tuungane na #TokomezaUharibifuWaMazingiraWaTakaZaPlastiki kwa manufaa ya mazingira yetu na viumbe vya baharini.