MAKAMUN WA RAIS MPANGO AISIFIA SIKU YA BAHARI DUNIANI.

15 Jun, 2023 08:00 AM-O3:00 PM Dar es Salaam
MAKAMUN WA RAIS MPANGO AISIFIA SIKU YA BAHARI DUNIANI.

Makamu wa Rais Mhe. Dr. Philip Isdor Mpango ameyapongeza maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani na waliohusika kuyaandaa maadhimisho ambapo amesema wameipa heshima inayoyostahili siku hii na kuweka wazi angependa maadhimisho ya mwakani yawe makubwa zaidi hata ya haya.

Dr. Mpango hakusita kutoa pongezi za dhati kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Wadau wote waliohusika kuandaa maadhimisho haya hapa Nchini.

Alitoa pongeza hizo jana jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo ya kusherehekea Siku ya Bahari Duniani yaliyoandaliwa na Taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

"Kwa namna ya pekee napenda kuipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi na wadau wote kwa kuandaa maadhimisho haya hapa nchini kwa mara ya kwanza hongereni sana. Hii ni hatua kubwa sana nami nafurahi kuungana nanyi kuadhimisha Siku ya Bahari ambayo kama tulivyoambiwa yanaadhimishwa kila mwaka tarehe kama ya leo 08/06 kila mwaka na tumeambiwa pia wazo hili lilipendekezwa mwaka 1992 lakini hatimaye lilitambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa mwaka 2002.

Aidha, Dkt. Mpango katika kuhakikisha maadhimisho haya yanazidi kuwa makubwa na kupata kutambulika zaidi aliomba kutoa rai kwa kuwaomba waandaaji wa shughuli hii wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani kwa mwakani yawe makubwa zaidi.

"Tuangalie uwezekano wa kupata wavuvi au viongozi wao tupate viongozi hata wa masoko ya samaki na kama ikiwa Dar es Salaam najua kuna 'Fish Market' hapa lakini kuna wanavyuo na wanafunzi wengi vijana maana tunalinda bahari kwa ajili ya vizazi vijavyo kwa hiyo ni muhimu sana jambo hili ni kubwa" aliongezea Dk. Mpango.

Kauli mbiu ya Siku ya Bahari Dunia (2023) iilikuwa inasema "Planet Ocean: tides are changing".