NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA OFISI ZA MPRU.
NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA OFISI ZA MPRU.

Tarehe Iliyochapishwa: Jumapili, Septemba 24, 2023

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk.Daniel Elius Mushi ametembelea Ofisi za hifadhi za Bahari na Maeneo na Tengefu (MPRU) kwa ziara fupi ya kufanya kikao kwaajili ya maandalizi ya Mafia Festival 2023 yanayotarajia kufanyika kuanzia Septemba 28 mpaka septemba 30, 2023 katika Wilaya ya Mafia iliyopo Mkoa wa Pwani.

Dr. Mushi alifika katika ofisi hizo na kupokelewa na mwenyeji wake Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Dkt. Immaculate Sware Semesi ambapo walifanya kikao  kilichoshirirkisha  Viongozi wengine mbalimbali akiwemo DAS wa Wilaya ya Mafia Bw.  Zephania Sumaye pamoja na viongozi wengine kutoka  Bodi ya Wajumbe wa Udhamini ya MPRU.

Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Mafia Festival 2023 natarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bw. ambapo pia kutakuwapo na matukio mengine ya burudani pamoja na michezo mbalimbali kwa watakaoweza kushiriki ambapo wasanii mbalimbali wanatarajia kutumbuiza katika tamasha hilo.

Maadhimisho haya yanatarajia kuwa chachu ya kuinua uchumi kwa shughuli mbalimbali za utalii katika Kisiwa cha Mafia pamoja na kutoa fursa kwa wakazi wa Wilaya ya Mafia na maeneo mengine ya jirani kuja kujuonea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Kisiwa hicho.