DKT. BAYA AMPONGEZA MPOTWA KWA NZURI, AAHIDI KUMPA USHIRIKIANO MENEJA MPYA MPRU
Jumamosi, Februari 28, 2026, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hifadhi za Bahari Maeneo Tengefu (MPRU) Dkt. Bonaventure Baya anempongeza aliyekuwa Kaimu Meneja wa MPRU Bw. Davis Mpotwa kwa kazi nzuri aliyoifanya alipokuwa akiongoza taasisi hiyo katika kipindi cha mpito.
Dkt. Baya aliyasema hayo tarehe 27, Februari 2026 katika hafla ya makabidhiano ya ofisi kwa Meneja mpya yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya MPRU jijini Dar es Salaam.
“Ni kumshukuru tu kwa kweli mwenzetu kwa kazi aliyoifanya sio ndogo kwani kazi aliyoifanya ni ngumu sana” Alisema Dkt. Bonaventure Baya.
Aidha, Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wadhamini ya MPRU pia alimpongeza Meneja mpya Dkt. Emmanuel Sweke kwa uteuzi wake na kuahidi kumpa ushirikiano mzuri kutoka kwa Bodi ya Wadhamini.
Halikadhalika, Aliyekuwa akikaimu nafasi ya Meneja Bw. Davis Mpotwa aliwashukuru Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Menejimenti, na Watumishi wa MPRU kwa ujumla kwa ushirikiano wao waliompatia katika kipindi chake cha uongozi.
Kwa upande wake, Meneja wa MPRU Dkt. Emmanuel Swege amemshukuru Bw. Mpotwa kwa kufanya kazi nzuri katika kipindi alichohudumu katika nafasi hiyo vilevile amemshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MPRU Dkt. Bonaventure Baya kwa ushiriki wake katika hafla hiyo ya makabidhiano.
“Naomba sana sana kutoka ndani ya moyo wangu nimshukuru sana kaka Davis Mpotwa kwa kufanya kazi ambayo ni nzuri alipokaimu kwa miaka miwili, hatukuwahi kusikia kuna migogoro hapa MPRU wala kesi zozote” alisema Dkt. Swege.

