DKT SWEKE ASISITIZA ELIMU YA UHIFADHI SABA SABA DAR
DKT SWEKE ASISITIZA ELIMU YA UHIFADHI SABA SABA DAR

Jumatatu, Julai 6, 2026. Dar es Salaam

Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Dkt. Emmanuel Sweke, ametembelea banda la MPRU leo Julai 6, 2026, katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, ambavyo ni mwenyeji wa Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Saba Saba).

Dkt. Sweke akizingumza na wataalamu wa MPRU amesisitiza juu ya umuhimu wa kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa vitendo kwa wananchi ili kuongeza uelewa wa jamii kuhusu mchango wa uhifadhi katika maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi wa buluu.

 

Katika maonesho hayo MPRU imeendelea kutoa elimu juu ya uhifadhi wa bahari, matumizi endelevu ya rasilimali za bahari, shughuli mbadala za kiuchumi kwa jamii za pwani, utalii wa kiikolojia pamoja na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika maeneo ya hifadhi za bahari.

Katika Msimu huu wa Sherehe za Saba Saba MPRU inaendelea kuwakaribisha wageni wote wa Maonesho ya Saba Saba kutembelea banda lake lililopo eneo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kujifunza zaidi kuhusu shughuli zake pamoja na fursa zilizopo katika sekta ya uhifadhi wa bahari, sambamba na kutembelea vivutio vya Hifadhi ya Bahari yakiwemo Maeneo Tengefu ya Dar es Salaam inayojumuisha visiwa vya Mbudya, Bongoyo na Sinda.

slot gacor