Dr. MAKAME ASISITIZA ZOEZI LA UTOAJI WA ELIMU KUHUSU UMUHIMU WA UTUNZWAJI WA MATUMBAWE
Dr. MAKAME ASISITIZA ZOEZI LA UTOAJI WA ELIMU KUHUSU UMUHIMU WA UTUNZWAJI WA MATUMBAWE

Ijumaa, Mei 16, 2025, Zanzibar

Mkurugenzi wa Idara ya Uhifadhi wa Bahari kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dk. Makame Omar Makame amewataka Maofisa wa Uvuvi, Mameneja wa Hifadhi za Bahari pamoja na Wananchi kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuhifadhi Matumbawe baharini ili kuongeza uzalishaji wa samaki katika maeneo hayo.

Dr. Makame ameyasema hayo Skuki ya Tumekuja, Wilaya ya Mjini wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya warsha ya utunzaji wa Matumbawe baharini.

Amesema matumbawe ya bahari yanapotumiwa vibaya na wavuvu samaki wanaozaliwa hupunguwa wakati wavuvi  wanapofanya shuhuli zao hasa Uvuvi wa nyavu za kukokota hivyo aliwataka kutoa elimu lengo kuona kila mvuvi na mtumiaji wa Bahari anatunza matumbawe.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Uhifadhi wa Matumbawe (CRRI) ambae pia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) Bw. Gedfrey Ngupula amesema lengo la mkutano huo kwa makundi hayo ni kuona wavuvi wanakuwa na uelewa wa kulinda na Matumbawe kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae.

Nao washiriki wa mkutano huo wamesema wamenufaika na mafunzo ya mkutano kwani wamepata uelewa wa kutuza matumbawe kwenye maeneo ya Hifadhi za Bahari.

Mkutano huo wa siku moja wa kuwajengea uwezo wasimamizi wa maeneo ya Baharini uliwashirikisha zaidi ya watu 100 na umelenga kutoa uelewa kwa jamii juu ya utunzaji wa Matumbawe baharini.