DR. MUYUNGI ATEMBELEA OFISI YA HIFADHI ZA BAHARI NA MAENEO TANZANIA MAKAO MAKUU
DR. MUYUNGI ATEMBELEA OFISI YA HIFADHI ZA BAHARI NA MAENEO TANZANIA MAKAO MAKUU

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatatu, Octoba 02, 2023

Mshauri wa Rais, Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira Dkt. Richard Stanislaus Muyungi leo Octoba 2, 2023 amefanya ziara fupi kwa kutembelea Ofisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Makao Makuu yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Dkt. Muyungi alipokelewa na vyema na mwenyeji wake Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tanzania Dkt. Immaculate Sware Semesi katika ofisi yake na kubadilishana maneno machache ya ukaribisho na ujio wake. Dkt. Muyungi alipata nafasi ya kufanya kikao na Menejimenti ya MPRU kuhusiana na masuala mazima ya Uhifadhi hususan masuala ya Bahari.

Aidha, Dkt. Muyungi ambaye ni  Mtaalam kuhusiana na masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira kupitia kikao hicho na menejimenti ya MPRU inaweza kuongeza chachu katika masuala ya Uhifadhi hususan sera ya uchumi wa buluu inayotiliwa mkazo na serikali.