ULEGA AKABIDHI BOTI  (11) ZA KISASA KWA WAVUVI WA DAR ES SALAAM
ULEGA AKABIDHI BOTI  (11) ZA KISASA KWA WAVUVI WA DAR ES SALAAM

Tarahe Iliyochapishwa: Jumanne, Novemba 28, 2023

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amekabidhi boti (11) za kisasa zenye thamani ya Shilingi ya Bilioni 1.85 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa mkopo kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo.

 Watumishi kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania walipata fursa ya kuhudhuria zoezi hilo la ugawaji wa boti hizo za kisasa kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Ulega  amemuelekeza Mkurugenzi wa Uvuvi kuhakikisha anatokomeza uvuvi haramu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka nyingine zinazohusika.

Mhe. Ulega ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa Uvuvi ya kukithiri kwa vitendo vya Uvuvi haramu katika ukanda wa Pwani hususani Dar es Salaam.