HAZINA YA BIOANUAI NA FURSA ZA UTALII ENDELEVU KUSINI MWA TANZANIA KISIWA CHA KISIWA KIDOGO
HAZINA YA BIOANUAI NA FURSA ZA UTALII ENDELEVU KUSINI MWA TANZANIA KISIWA CHA KISIWA KIDOGO

Jumanne      Aprili 21 2026. Mtwara

Kisiwa Kidogo ni miongoni mwa visiwa vya kipekee vilivyopo ndani ya Hifadhi ya Bahari ya Huba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma (MBREMP). Kisiwa hiki kina umuhimu mkubwa wa kiikolojia, hususan uhifadhi wa ndege wa aina mbalimbali na bioanuai za baharini.

 

Kikiwa na mandhari ya kuvutia ya miamba, Kisiwa Kidogo kimezungukwa na mazingira yanayovutia utafiti, utalii na wadau wa mazingira. Umuhimu wake katika kulinda viumbe hai unaenda sambamba na mchango wake katika kukuza utalii unaozingatia misingi ya uhifadhi.

Aidha, kisiwa hiki kina fursa mbalimbali za uwekezaji katika utalii endelevu, zinazoweza kuchangia maendeleo ya kiuchumi huku zikihifadhi rasilimali za bahari.

 

Kupitia story map hii, Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) inakukaribisha kujifunza zaidi kuhusu Kisiwa Kidogo; kuanzia mazingira yake ya asili, nafasi yake katika uhifadhi wa bioanuai, hadi mchango wake katika maendeleo ya utalii endelevu kusini mwa Tanzania.

Bofya link hii ili kutzama;

https://uploads.knightlab.com/storymapjs/c35a375f70683c46293332119bfad813/kisiwa-kidogo-tanzania-s-secret-rocky-bird-santcuary/index.html