WAZIRI ULEGA, MPRU WAKUTANA NA MKURUGENZI 'WORLDFISH'
WAZIRI ULEGA, MPRU WAKUTANA NA MKURUGENZI 'WORLDFISH'

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatatu, Disemba 04, 2023

Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) pamoja na Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Dr. Immaculate Sware (kulia) wakutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa WorldFish, Dkt.  Essam Yassin Mohammed  (kushoto), pembezoni mwa Mkutano wa COP 28 Dubai, UAE.

WorldFish ni taasisi ya kimataifa yenye makao yake makuu nchini Malaysia, inashughulika na utafiti na ubunifu katika minyororo ya thamani ya  uvuvi na ukuzaji viumbe.

Katika mazungumzo yao Mhe. Ulega amemwelezea Mkurugenzi huyo kuhusu nia ya Tanzania kushirikiana na WorldFish katika kuimarisha Sekta ya Uvuvi ili iwe na mchango mkubwa zaidi kwa taifa.