UZINDUZI WA KAMATI TENDAJI YA MRADI WA CRRI
UZINDUZI WA KAMATI TENDAJI YA MRADI WA CRRI

Jumanne 06, Februari 2024, Morogoro

Katibu Mkuu Wizara Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Silas Shemdoe amezindua kamati tendaji ya mradi wa kuokoa miamba ya matumbawe ujulikanao kama Coral Reef Rescue Initiative Project (CRRI). Mradi huu unatekelezwa katika maeneo ya Hifadhi za Bahari, ambapo Taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) imepewa dhamana ya kusimamia na kutekeleza mradi huo. Kamati hio ya kitaifa inafahamika kama 'National Steering Committee', imepewa majukumu mbalimbali ya uzimamizi wa mradi ikiwemo kupitia bajeti za mradi, kupitia taarifa za mradi, kushauri kuhusu namna bora ya utekelezaji wa miradi.