“MAFIA NI ENEO LA KIPAUMBELE KATIKA UTALII”- RC KUNENGE.
“MAFIA NI ENEO LA KIPAUMBELE KATIKA UTALII”- RC KUNENGE.

Tarehe Iliyochapishwa: Alhamisi, Septemba 28, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Aboubakar Kunenge, amesema kwamba eneo la Kisiwa cha Mafia ni kipaumbele katika shughuli za kiutalii katika Mkoa wa Pwani.

Mhe. Kunenge ameyasema hayo leo tarehe 28 Septemba alipokuwa akifungua Maonesho ya Utalii, Biashara na Uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya Mafia Lodge, Utende. 

Maonesho haya yameanza rasmi leo na kutarajiwa kuhitimishwa Septemba 30, 2023 ambapo pia kulikuwa na shughuli mbali mbali kuweka utimamu wa mwili kama kukimbia (marathon), kuendesha baiskeli, ngalawa, kuogelea. 

Aidha, kupitia maonesho haya watalii wa nje na wa ndani watapata kujionea na kujifunza vivutio vinavyopatikana katika Kisiwa cha Mafia pamoja na kusaidia kukuza shughuli za kiuchumi nchini.