MBREMP YAZINDUA MSIMU WA NYANGUMI MTWARA.
MBREMP YAZINDUA MSIMU WA NYANGUMI MTWARA.

Taarehe Iliyochapishwa: Jumamosi, Agosti 05, 2023

Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingiliano ya Mto Ruvuma (MBREMP) leo wamefanya
hafla ya uzinduzi wa Msimu wa Nyangumi iliyofanyika katika kata ya Msimbati katika mkoa wa
Mtwara.
Hafla hiyo ya uzinduzi wa msimu mpya wa Nyangumi ilisimimiwa chini ya Hifadhi za Bahari na
Maeneo Tengefu kwa kushirikiana na “Visit Mtwara” kufanikisha tukio hilo.
Uzinduzi huu umefanywa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Bw.Kanali Ahmed Abbas
ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa tukio hilo la Uzinduzi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali
kutoka Mtwara.
Mgeni rasmi Mhe. Bw. Kanali Ahmed Abbas amesema kuwa utawekwa mpango mkakati
madhubuti wa kuhakikisha unachochea kukuza utalii katika Mkoa huo wa Mtwara na kusaidia
kukuza uchumi kupitia watalii.
Kauli mbiu ya Uzinduzi huu wa Msimu wa Nyangumi ni “Wekeza, Tembelea, tukuze Mtwara
yetu”.