MBREMP WATOA ELIMU YA UHIFADHI WA BAHARI NA MAZINGIRA KWA WANAFAUNZI WA SEKONDARI MSIMBATI

Jumanne, Machi 11, 2025, Mtwara
Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma (MBREMP) kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii Mnazi Bay imetoa elimu kuhusu Uhifadhi wa Bahari na mazingira kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Msimbati iliyopo mkoani Mtwara.
Zoezi hilo la utoaji elimu ya kuwajengea uelewa wanafunzi hao iliongozwa na Ndg. Mwahija Alawi, Sospiter Wambura pamoja na Stellah Masai ambapo wanafunzi takribani 98 kutoka Shule ya Sekondari ya Msimbati waliweza kupatiwa elimu hiyo ya Uhifadhi wa Bahari na mazingira.
Moja ya jukumu kubwa kwa Idara ya Maendeleo ya Jamii Mnazi Bay kwenye Maeneo yaliyohifadhiwa ya Bahari (MPAs) ni kuhakikisha jamii inajengewa uelewa juu ya Uhifadhi wa Bahari na mazingira pamoja na kukuza juhudi za Uhifadhi shirikishi, matumizi endelevu ya Rasilimali za Bahari, kukuza fursa za Uchumi wa Buluu, uwekezaji na utalii wa Bahari.
Aidha, Idara hiyo imekusudia mpaka kufikia 2026 takribani asilimia 90 ya watu wanaioishi ndani na nje ya Hifadhi kupata uelewa juu ya elimu ya Uhifadhi na viumbe maji Ili kupunguza matumizi ya dhana haramu za uvuvi na ukataji wa mikoko.