WATUMISHI KUTOKA MIMP NA MBREMP WANG'ARA KATIKA UPIGAJI MAJI WAZI NA MAFUNZO YA EFR
WATUMISHI KUTOKA MIMP NA MBREMP WANG'ARA KATIKA UPIGAJI MAJI WAZI NA MAFUNZO YA EFR

Jumatatu, 25 Machi 2024, Mafia

Watumishi wawili wa Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP) na Hifadhi ya Bahari ya Mnazi Bay na Maingiliano ya Mto Ruvuma (MBREM), Bw. Daniel Malya na Bw. Mustapha Issa ni kati wa watumishi wawili waliofanya vyema katika mafunzo ya 'Open Water Diving’.

Halikadhalika, watumishi watatu kutoka MIMP, Dkt. Kulwa Mtaki, Bw. Paschal Mkongola, na Bw. Bernard Ngatunga, walifanya vyema katika kozi ya 'Emergency First Rescue' (EFR).

Mafanikio haya yanaashiria mwanzo wa sura mpya kwani wiki ijayo, wataungana na Mzamiaji Mbobezi, Bw. Masanja Joram, kutoka MIMP ili kuendeleza ujuzi wao katika 'Advanced Open Water Diving' na Uzamiaji wa Uokozi. 

Mafunzo hayo yanayoongozwa na Plongeurs du Monde (Flabelline Mission) kwa kushirikiana na MIMP na Kituo cha Mafunzo ya Uzamiaji cha Mafia yanasisitiza dhamira ya kujenga uwezo. 

Mpango huu, unaoungwa mkono na Menejimenti ya MPRU, hautumiki tu kama chanzo cha motisha lakini pia huongeza uwezo kwa Wahifadhi Wafawidhi, na kuchangia mafanikio ya jumla ya juhudi za Uhifadhi..