TAKWIMU ZA UVUVI MIMP SASA NI KWA eCAS
TAKWIMU ZA UVUVI MIMP SASA NI KWA eCAS

Tarehe Iliyochapishwa: Jumanne, Octoba 17, 2023

Siku 10 za mafunzo ya kujenga uwezo wa kukusanya takwimu za mazao ya uvuvi kidigitali Kwa kutumia mfumo wa eCAS , yameanza siku ya jumatatu tarehe 16/10/2023, katika Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa Cha Mafia.

 Jumla ya washiriki 14 wanajengewa uwezo ikiwa ni pamoja na Wakusanya Takwimu ( Data enumerators) kutoka vijiji 5 vya Kiegeani, Chemchem, Bwejuu, Miburani na Jibondo. Pamoja nao wapo Wahifadhi 6, Afisa Uvuvi 1 na Afisa Tehama 1 Bw. Abbas Maige kutoka Hifadhi za Bahari na Maneneo Tengefu Tanzania.

Mafunzo haya ambayo yanahusisha nadharia na kazi za uwandani yatawezesha takwimu za uvuvi za ndani ya Hifadhi Kwa mara ya kwanza kuingia na kupatikana kwenye Mfumo wa Taifa wa Takwimu za Uvuvi. Wawezeshaji kutoka Idara ya Takwimu ya Wizara na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania ( TAFIRI) wamelenga kutoa mafunzo haya ili kuwafanya Washiriki kuwa na uwezo wa kufundisha wengine (ToT).

Mradi wa BAF kupitia WWF wamewezesha kufanyika Kwa mafunzo haya ikiwa ni pamoja na manunuzi ya vifaa mbalimbali ambavyo ni Laptop1,Simu Janja 10, Mizani 10 na mabegi 8 yasiyopitisha maji. Takwimu za samaki ni muhimu katika kuweka vipaumbele na mipango mbalimbali ya maendeleo na uhifadhi baada ya kujua Hali ya afya ya Bahari na mchango wake kwenye uchumi wa nchi na jamii husika .