MIMP YAFANYA MKUTANO WA MPANGO WA URASIMISHWAJI KWA VIWANGO VYA TOZO
MIMP YAFANYA MKUTANO WA MPANGO WA URASIMISHWAJI KWA VIWANGO VYA TOZO

Monday, 26 February 2024, Mafia

Timu ya Wataalam kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) ikiongozwa na Maafisa Sheria, Bw. Chaila Lupindu pamoja na Bw. Wilfred Msagati kwa kushirikiana na Muhasibu Bw. Sweetbert Francis wamefanya mkutano na wadau wa Utalii kutoka Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP) kurasimisha mpango wa viwango vya  tozo mbalimbali ndani ya Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia.

Halikadhalika, kwa  upande wa MIMP waliongozwa na Mhifadhi Mfawidhi (WIC), Bw. Amin Abdallah na Mhifadhi, Bw. Mohamed Shamte ambao walishiriki vyema katika mkutano huo.