MKURUGENZI WA HALMASHAURI MTWARA ASHIRIKI ZOEZI LA USAFI NA KUPANDA MIKOKO MBREMP SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI MTWARA ASHIRIKI ZOEZI LA USAFI NA KUPANDA MIKOKO MBREMP SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Alhamisi, June, 05, 2025, Mtwara

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Ndg. Abeid A. Kafunda ameshiriki zoezi la usafi wa mazingira na kupanda mikoko katika fukwe za Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingiliano ya Mto Ruvuma (MBREMP) katika Kijiji cha Msimbati, Mkoani Mtwara.

Zoezi hilo la usafi na upandaji wa mikoko limefanyika June 05, 2025 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Mtwara ambaye alishirikiana na wadau kutoka M&P, Indian Ocean Conservation Alliance’ (IOCA), wanafunzi pamoja na viongozi wa kijiji kutekeleza zoezi hilo.

MBREMP walishiriki zoezi hilo wakiongozwa na Mhifadhi Mfawidhi Dkt. Redfred Ngowo akiwa na wafanyakazi wengine ambapo kwa pamoja walishirikiana katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani yenye kauli mbiu isemayo “Mazingira Yetu na Tanzania ijayo Tuwajibike sasa; Dhibiti Matumizi ya Plastiki".