MPRU WASHIRIKIANA NA PLONGEURS DU MONDE KUTOA MAFUNZO YA UZAMIAJI KWA WATUMISHI WA HIFADHI YA BAHARI YA KISIWA CHA MAFIA.
MPRU WASHIRIKIANA NA PLONGEURS DU MONDE KUTOA MAFUNZO YA UZAMIAJI KWA WATUMISHI WA HIFADHI YA BAHARI YA KISIWA CHA MAFIA.

Tarehe Iliyochapishwa: Jumanne, Mei 16, 2023

Plongeurs du Monde ni Taasisi isiyo ya Kiserikali na inayoendesha shughuli zake bila kutengeneza faida.Taasisi hiyo yenye makazi yake Ufaransa imekuwa ikijenga uwezo wa jamii za watu wa mwambao wa nchimbalimbali duniani kwenye eneo la Uzamiaji (Diving), Tanzania ikiwa ni mojawapo. Kisiwa cha Mafia na hasandani eneo la Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia mafunzo yamekuwa yakifanyika kila mwaka.

Uongozi wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania ambayo imekuwa ikishirikiana kwa ukaribu na Taasisi hiyokutoka Ufaransa, ili kuwezesha watumishi waliomo ndani Hifadhi kupata mafunzo ya Uzamiaji na kujengewa uelewa na umuhimu wa maisha ya chini ya Bahari ili wawe Mabalozi wa Uhifadhi kwa wananchi wengine. Maamuzi haya ya kujengea uwezo kwa watumishi yana manufaa makubwa kwa maslahi ya taasisi hasakwenye shughuli mbalimbali za ufatiliaji wa rasilimali za chini ya Bahari (Benthic Monitoring), Upandaji wa Mtumbawe (Coral Restoration) na Uokoaji (Rescue).

Halikadhalika, ngazi ya "Dive Master" ni muhimu sana hasa kwenye masuala mazima ya usimamizi na uendeshaji wa "Diving Center"  na Utalii wa Kuzamia. Hii ni moja ya hatua kubwa iliyofanywa na Taasisi inapofuata kuongeza vyanzo vya mapato, uanzishaji wa "Diving Center" utapelekea katika kutimiza lengo hilo na hapo umuhimu wa 'Dive Master" unapohitajika kwani ndiyo ngazi inayotambuliwa kimataifa katika kuongoza watalii, usimamizi na uendeshaji wa "Diving Center" kibiashara na kwa kuzingatia vigezo vya usalama. 

Wahitimu waliohitimu ngazi mbalimbali wameshukuru na kupongeza hatua hii inayoendelea kuchukuliwa na Menejimenti ya MPRU.Kwa upande wa watumishi, MPRU imewezesha kujengewa uwezo wa taaluma hiyo ya ujuzi wa Kuzamia (Diving) kwa watumishi wapatao 8 kutoka vituo vyake vyote 4 ndani ya miaka 2. Mafunzo hayoyalihitimishwa 07/04/2023. Watumishi hao ni pamoja na;

A .Rescue Diver Level

1. Nelson Mdogo-TACMP (2021-2023) Kuanzia Open Water Diver

2.Davis Orio-MBREMP (2021-2023) Kuanzia Open Water Diver 

3. Amos Singo-MREMP (2021-2023) Kuanzia Open Water Diver

4. Masanja Joram-MIMP (2022-2023) Kuanzia Advance Open Water Diver hadi Dive Master Theory

B. Advanced Open Water Diver Level

1. Dr. Kulwa Mtaki-MIMP

2. Paschal Mkongola-MIMP

3. Bernad Ngatunga-MIMP kuanzia Open Water Diver 2023.

C. Dive Master Level

1. Pagu Julius-DMRS Dive Master 2022-2023.