MPRU NDANI YA FORBES AFRICA
MPRU NDANI YA FORBES AFRICA

Tarehe Iliyochapishwa: Alhamisi, Januari 25, 2024

Kaimu Meneja Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Bw. Davis Mpotwa amekutana na Mwakilishi wa Jarida la Forbes Bi. Julian, kwa majadiliano juu ya ushirikiano kati ya Taasisi ya MPRU na gazeti hilo.

Ushirikiano huo umelenga kuchapisha Makala mbalimbali za Uhifadhi wa rasilimali za Bahari pamoja na utalii wa bahari, kupitia ushirikiano huu shughuli za Uhifadhi za utalii zinaenda kutangazwa miongoni mwa nchi za Afrika ambapo Jarida hilo maarufu la Forbes linafika.

Jarida la Forbes limejikitika sana katika utoaji wa takwimu, orodha na madaraja na vitumbalimbali, kadhalika jarida hili huangazia maswala ya fedha, viwanda, uwekezaji na masoko. Kupitia wasomaji wake wengi walioenea duniani kote ujumbe huu mahususi wa utunzaji wa mazingira utaifikia jamii ya dunia nzima sambamba na kuhamasisha uwekezaji katika rasilimali za bahari na vivutio mbalimbali vya bahari.