MENEJA MPRU AKUTANA NA MKUU WA WILAYA YA MAFIA MHE. SUMAYE.
MENEJA MPRU AKUTANA NA MKUU WA WILAYA YA MAFIA MHE. SUMAYE.

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatatu, Septemba 25, 2023

Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania Dr.Immaculate Sware Semesi na Mhifadhi Mfawidhi Hifadhi za Bahari Mafia, Bw. Amini Abdallah pamoja na wafanyakazi wa Hifadhi za Bahari Mafia wamekutana na kufanya kikao na Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Mh.Zefania Sumaye na Mkurugenzi wa Halmashauri Mh. Ndumbo leo tarehe Septemba, 25,2023 katika Ofisi ya Wilaya ya Mafia.

 Kikao hiko ni katika kujadili mwenendo wa Maadhimisho ya Uzuri na vivutio vya Kisiwa Cha Mafia ama kama ijulikanavyo kama Mafia Festival2023 ambako Maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia Tarehe 28-30 Septemba 2023 katika Hifadhi za Bahari Mafi.

 Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) tunawakaribisha Watanzania wote na wageni wote kufika Kisiwani Mafia na ndani ya Hifadhi ya Bahari Mafia kufurahia vivutio vya Bahari na kuelimika katika Uhifadhi wa Bahari.