MPRU NA WWF WAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIKANDA
Jumatatu, Mei 11, 2026, Dar es Salaam
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) imepata nafasi ya kumpokea Bi. Yvonne Godo katika ziara yake ya kwanza rasmi akiwa Mkurugenzi wa WWF Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Katika ziara hiyo, Bi. Godo alikutana na Uongozi wa WWF Tanzania na kushiriki majadiliano na wadau muhimu wa serikali, wakiwemo Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) pamoja na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika juhudi za uhifadhi wa mazingira na rasilimali asilia nchini.
Majadiliano haya yamelenga kuendelea kuimarisha ushirikiano thabiti kati ya WWF na Serikali ya Tanzania, sambamba na dhamira ya pamoja ya kuhifadhi urithi wa asili wa taifa, ikiwemo Hifadhi ya Bioanuai ya RUMAKI.
Ziara hio pia imeonesha umuhimu wa juhudi za uhifadhi nchini Tanzania ngazi ya kikanda, na sambamba na dhamira ya pamoja ya WWF ya kuendeleza uhifadhi unaozingatia mazingira, ustawi wa jamii na himilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

