MPRU YAADHIMISHA SIKU YA BAHARI DUNIANI KWA USAFI WA FUKWE NA UPANDAJI MIKOKO TANGA
MPRU YAADHIMISHA SIKU YA BAHARI DUNIANI KWA USAFI WA FUKWE NA UPANDAJI MIKOKO TANGA

Jumatatu    Juni 08, 2026     Tanga

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU), kupitia Hifadhi ya Bahari ya Silikanti Tanga, imeungana na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa mazingira ya bahari kuadhimisha Siku ya Bahari Duniani kwa kufanya shughuli za usafi wa fukwe na upandaji wa mikoko katika Mtaa wa Mnyanjani, Kata ya Mnyanjani, Wilaya ya Tanga Mjini.

 

Maadhimisho hayo yalifadhiliwa na Shirika la GIZ na kushirikisha Kamati ya Hifadhi ya Jamii (VLC) ya Mnyanjani, wananchi wa eneo hilo pamoja na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa mazingira ya bahari wakiwemo Mwambao Coastal Community Network, WCS na Blue Vision.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga Mhe. Angela Mono ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, wadau wa maendeleo na jamii katika kulinda mifumo ikolojia ya bahari ili kuhakikisha rasilimali hizo zinaendelea kutoa manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho.

 

Mbali na shughuli za uhifadhi, maadhimisho hayo yalifuatiwa na maonesho ya sanaa kutoka kwa wanafunzi wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Msingi Mnyanjani, ambao waliwasilisha mashairi na ngonjera zenye ujumbe wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira ya bahari na rasilimali zake kwa matumizi endelevu

 

Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yamelenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa bahari katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, usalama wa chakula, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na uhifadhi wa bioanuwai za baharini. Kaulimbiu ya mwaka huu imehimiza kuchukuliwa kwa hatua za pamoja katika kulinda afya ya bahari kwa mustakabali endelevu wa dunia.

slot gacor