MPRU YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI 2024)
MPRU YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI 2024)

Jumatano, 01 Mei 2024, Dar es Salaam

Watumishi kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) wameungana na Wafanyakazi wote Duniani kusherekea Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) zilizofanyika katika viwanja vya Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Mei, 2024.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila alikuwa mgeni rasmi kwa mwaka huu katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo “Nyongeza ya Mshahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”. 

"Suala la kuongeza mishahara ni suala ambalo Mheshimiwa Rais analifanyia kazi ili kuboresha maslahi ya kila manyakazi na hivyo kupunguza ugumu wa maisha" alisema Mhe. Chalamila wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika kimkoa katika Uwanja wa Uhuru. 

Kauli mbiu kutoka Hifadhi za Bahari  na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) ilikuwa ni “Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Bahari kwa Ukuaji wa Uchumi wa Buluu”.