MPRU YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA 49 SABASABA 2025

Jumatano, Agosti 13, 2025, Dar es Salaam
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) imeshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 49 (Sabasaba) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, ikiwa ni jitihada za kuonyesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi hiyo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
Wawakilishi waliokuwepo kwenye Banda la MPRU akiongozwa na Afisa Masoko, Halima Tosiri, Afisa Uhusiano, Bw. Ivan Kimaro pamoja na wengine waliweza kutoa elimu kuhusiana na shughuli zinazofanywa na Taasisi ikiwemo Uhfadhi wa Bahari na utunzaji wa rasilimali zake kama vile mikoko, matumbawe na jinsi kulimo cha mwani kinavyoweza kuzalisha fursa za kibiashara kwa wajasiriamali na kuinua uchumi wa Mtanzania katika jitihada za kuinua Uchumi wa Buluu nchini.
Maonesho hayo ya Sabasaba ni fursa ya kipekee kwa MPRU kuwasiliana moja kwa moja na wananchi na wadau mbalimbali wa Utalii hususan katika utalii wa Bahari ili kuboresha utoaji wa huduma na kuelimisha kuhusu umuhimu wa Uhifadhi wa Bahari katika kuendeleza na kukuza sera ya Uchumi wa Buluu nchini kwa pamoja.