MPRU YASHIRIKI MKUTANO WA 11 WA ‘OUR OCEAN CONFERENCE’ NCHINI KENYA, TANZANIA YATANGAZA NIA YA KUANZISHA HIFADHI YA BAHARI YA KILWA
MPRU YASHIRIKI MKUTANO WA 11 WA ‘OUR OCEAN CONFERENCE’ NCHINI KENYA, TANZANIA YATANGAZA NIA YA KUANZISHA HIFADHI YA BAHARI YA KILWA

Jumatatu, Juni 22, 2026, Mombasa - Kenya

Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu  (MPRU) imeshiriki kikamilifu Mkutano wa 11 wa ‘Our Ocean Conference’ uliofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 18 Juni 2026 Mombasa, Kenya, ambapo ni mkutano wa kwanza wa aina yake kufanyika barani Afrika. Mkutano huo uliwakutanisha viongozi wa serikali, wataalamu na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa bahari kutoka duniani kote kujadili mustakabali wa rasilimali za bahari na matumizi yake endelevu.

Ujumbe wa MPRU uliongozwa na Meneja wa MPRU, Dkt. Emmanuel Sweke akisaidiwa na Mhifadhi Mkuu, Bw. Godfrey Ngupula, Dkt. Kulwa Mtaki pamoja na Bw. Ailars Lema huku kwa upande wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu (Sekta ya Uvuvi), Prof. Mohamed Sheikh, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Katika mkutano huo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitangaza rasmi nia ya kuanzisha Hifadhi ya Bahari ya Kilwa (Kilwa Marine Park) ili kuimarisha uhifadhi wa bioanuai na usimamizi endelevu wa rasilimali za bahari nchini.

MPRU imeeleza kuwa hatua hiyo itaongeza mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa na kuimarisha mchango wa sekta ya uhifadhi wa bahari katika maendeleo ya uchumi wa buluu. Aidha, MPRU imeanza maandalizi ya awali ya utekelezaji wa uanzishwaji wa Hifadhi ya Kilwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi.

MPRU imeishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano wake na kusisitiza kuwa mafanikio ya mkutano huo yanafungua ukurasa mpya katika juhudi za Tanzania za kuhifadhi mazingira ya bahari kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

 

slot gacor