MPRU YASHIRIKI PROGRAMU YA MAFUNZO USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA BAHARI
Ijumaa, 29 Septemba 2024, Zanzibar
Menejimenti ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) ikiongozwa na Kaimu Meneja, Bw. Davis Mpotwa (watatu kutoka kushoto mstari wa mbele) imeshiriki mafunzo ya kujenga uwezo kuhusu programu ya ‘Adaptive Management’ iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar.
Programu hiyo ya mafunzo iliyoandaliwa na Wakala wa Usimamizi wa Bahari na Maji wa Uswidi (SwAM) ilifanyika kwa siku 5 kuanzia Novemba 21-27 ililenga utoaji wa mafunzo yaliyokusudia kuboresha ujuzi na mbinu za uhifadhi wa rasilimali za baharini kwa ufanisi.
Mpango huu ulikuwa hatua muhimu katika kuwawezesha watumishi wa MPRU kushughulikia changamoto katika usimamizi wa rasilimali za baharini ipasavyo huku ukisisitiza kujifunza kwa kushirikiana na kupitishwa kwa mbinu bora ili kupata matokeo chanya katika juhudi za uhifadhi.