BW. MPOTWA ATEULIWA KUWA KAIMU MENEJA MPRU
BW. MPOTWA ATEULIWA KUWA KAIMU MENEJA MPRU

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatatu, Januari 22, 2024

Menegimenti na Watumishi wa Taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) wanampongeza Bw. Davis Mpotwa kwa kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Dkt. Riziki Shemdoe kukaimu nafasi ya Meneja wa Taasisi ya MPRU.

Bw. Davis ni Mkuu wa Kitengo cha Utalii, Habari na Masoko MPRU. Uteuzi huu umeanza 20 Januari,2024.