BOTI YENYE KIOO MV DODOJI II
BOTI YENYE KIOO MV DODOJI II

Tarehe Iliyochapishwa: Ijumaa, Novemba 10, 2023

MV Dodoji II ni jina la Boti mpya ya kisasa yenye kioo inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni, itakayowezesha wageni na watalii kuona viumbe na mandhari ya ndani ya bahari.

Boti hii imepewa jina la samaki aitwaye Dodoji, samaki huyu ni kiumbe  wa kipekee mwenye muonekano kama mnyama Farasi ambae umbile lake hufikia hadi cm 35.

 Dodoji wanapatikana katika Hifadhi za Bahari ya Hindi Tanzania na makazi yake ni katika matumbawe, mikoko na nyasi bahari.

Kwa upekee wake Dodoji kuna umuhimu wa kutunza na kuhifadhi aina hii ya samaki, Boti yetu mpya na ya kisasa inakuja na jina la MV Dodoji II.