MWENYEKITI WA BODI YA MPRU AONGOZA KIKAO CHA KAWAIDA CHA BODI
MWENYEKITI WA BODI YA MPRU AONGOZA KIKAO CHA KAWAIDA CHA BODI

Ijumaa, Aprili 24, 2026, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Dkt. Bonaventure Baya, ameongoza kikao cha kawaida cha Bodi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi za Bunge Aprili 24, 2026 jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimelenga kupitia taarifa mbalimbali za utendaji wa taasisi, kwa lengo la kuimarisha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ili kuhakikisha kunakua na usimamizi bora wa rasilimali za bahari.

 

Aidha, Kikao cha bodi ni miongoni mwa majukumu ya msingi ya Bodi ya Wadhamini ya MPRU, ambayo ilizinduliwa Januari 2026 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ikiwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa shughuli za Taasisi, kutoa muelekeo wa kimkakati na kuidhinisha mipango mbalimbali ikiwemo mpango mkakati, bajeti na miradi ya kimkakati.