MPANGO UTEKELEZAJI WA KITAIFA WA ULINZI NA MPANGO WA UHIFADHI WA KASA WA BAHARINI
MPANGO UTEKELEZAJI WA KITAIFA WA ULINZI NA MPANGO WA UHIFADHI WA KASA WA BAHARINI

Ijumaa, 1 Machi 2024, Morogoro

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe ameshiriki kikao cha kupitia Mkakati wa mpango wa Kitaifa wa kulinda na kuhifadhi Kasa (Sea turtles), kilichofanyika Mkoani Morogoro.

Mpango huo unaofahamika kama "National Action Plan for Marine Turtles Protection and Conservation Plan" utekelezwaji wake unatarajiwa kuanza mwaka 2024-2029, pindi utakapotiliwa sahihi na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Kikao kimeshirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na KM Blue Economy, DFs, Sea Sense pamoja na MPRU ambao ndio wenyeji wa kikao hicho.