MAANDALIZI YA MAFIA KUELEKEA SIKU YA HIFADHI ZA BAHARI (MPAs 2023).
MAANDALIZI YA MAFIA KUELEKEA  SIKU YA HIFADHI ZA BAHARI (MPAs 2023).

Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa Cha Mafia jana tarehe 30/07/2023 Kwa ushirikiano mkubwa wa Kikundi Cha Akina Mama - (Uchumi wa Buluu) ,wameshiriki pamoja kufanya USAFI wa mazingira kwenye maeneo ya huduma za Jamii ya Zahanati na Shule ya Msingi Mlongo.

Kikundi hicho kinachojihusisha na uhifadhi na utoaji Elimu ya uhifadhi wa mazingira ya Bahari katika Kijiji Cha Mlongo wamejihusisha kikamilifu kwenye tukio hili wakiendana na kaulimbiu ya Kuadhimisha siku ya Hifadhi za Bahari Kwa ajili ya Jamii Kwa kushiriki usafiri kwenye Zahanati na Shule.

Pamoja nao Wanafunzi 11 kutoka vyuo mbalimbali walioko kwenye mafunzo Kwa vitendo,walishiriki . Wanafunzi hao ni kutoka  UDSM,FETA,IMS na NTC.Katika majadiliano baada ya kufanya USAFI ,Wanakikundi hao waliomba kuwezeshwa mafunzo ya Kilimo Endelevu Cha Mwani Ili waweze kujiongezea kipato.

Mhifadhi Shamte Mohamed aliwatoa hofu  Kwa kuwaahidi kulitekeleza jambo Hilo. Halikadhalika Mhifadhi Masanja Joram Kwa upande wake aliwaunganisha na Mwakilishi wa Kampuni ya Mwani Mariculture ambayo ni mnunuzi Mkuu wa Mwani na pia huwezesha vifaa vya Kilimo Cha Mwani ikiwemo kamba na taitai. Mwakilishi huyo aliahidi kuwatembelea Ili kuona ukubwa wa eneo walilochagua Kwa ajili ya Kilimo hicho.

Siku ya Hifadhi za Bahari ( MPAs Day) itafanyika tarehe 01/08/2023 na Kwa hapa nchini itaadhimishwa Kwa kufanya MKUTANO wa mtandaoni ( Virtual Conference). MKUTANO huu umeandaliwa na Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu ( MPRU) na Mgeni rasmi atakuwa ni Naibu Katibu Mkuu Uvuvi.