RAIS SAMIA AIPONGEZA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI, ARIDHISHWA NA KASI YA UTENDAJI WAKE.
RAIS SAMIA AIPONGEZA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI, ARIDHISHWA NA KASI YA UTENDAJI WAKE.

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatano, Januari 31, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu ametoa pongezi kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi inayoongozwa na Waziri Abdallah Ulega. Mhe. Dkt. Samia Suluhu amesema wizara ya kilimo na uvuvi imekua ikifanya mambo mengi makubwa na yenye kuleta tija kwa wananchi ambapo kupitia sekta ya uvuvi wananchi wengi wanategemea sekta hio kwa ajili ya kujipatia kipato.

Rais Samia amebainisha hayo jijini Mwanza wakati wa kukabidhi boti 160 na vizimba 222 kwa wanufaika kwenye kanda ya ziwa Victoria na kuitaka wizara kubuni mbinu zaidi za kuhakikisha inawezesha wanufaika zaidi kupitia rasilimali za uvuvi. Ambapo Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024 wizara hiyo ilipatiwa fedha Shilingi Bilioni 60 kila mwaka kwa miaka miwili mfululizo katika kukuza Sekta ya Uvuvi.

Aidha, Mhe. Ulega amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025 nia ya wizara ni kusambaza boti za uvuvi zisizopungua 500 kote nchini ili kuwezesha wanufaika wengi zaidi kwa kuwa Sekta ya Uvuvi inatoa ajira kwa zaidi ya watu Milioni 4.5. Halfa hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Kaimu Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bwana Davis Mpotwa.