TACMP YAPOKEA WAGENI KUTOKA HALMASHAURI YA KILWA NA BMU MTANDAO KUJIFUNZA SHUGHULI ZA UHIFADHI WA BAHARI

Alhamisi, Juni 26, 2025, Tanga
Menejimenti Hifadhi ya Bahari ya Tanga Silikanti (TACMP) chini ya Mhifadhi Mfawidhi Bi. Magreth Mchome umepokea ugeni kutoka Kilwa ambao ni Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi kwenye Mialo
(BMU) tofauti kutoka Kilwa wakiongozwa na Bw. Ulimboka Ndile kutoka Halmashauri ya Kilwa na Bw. Steven Yohana (BMU Mtandao).
Menejimenti hiyo ya TACMP ilipokea wageni hao kutoka Kilwa Juni 25, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya TACMP Mkoani Tanga chini ya Mhifadhi Mfawidhi Bi. Magreth Mchome ambapo lengo la ujio wa wageni hao ni kujifunza namna ambavyo TACMP inatekeleza shughuli za Uhifadhi na utalii kwa kuwashirikisha jamii na kuleta mafanikio chanya kwenye uhifadhi na kukuza vipato vya jamii.
Timu hiyo imepewa elimu hii ya Uhifadhi na wataalamu kutoka TACMP na kupewa fursa ya kujifunza zaidi kupitia VLC na uongozi wa serikali za mitaa kwakukutanishwa na kuelezwa namna kazi za kamati ya uhifadhi zinavyosaidia kuunganisha jamii katika kufanikisha shughuli za uhifadhi.
Ugeni huu umeambatana na mwakilishi kutoka Shirika la Mwambao, Bw. Kengela Mashimba ambao ni moja ya wadau wa kufanikisha shughuli za uhifadhi ndani ya MPRU.