TIMU YA MENEJIMENTI MPRU YAFANYA KIKAO KUJADILI MRADI WA CRRI AWAMU YA PILI
TIMU YA MENEJIMENTI MPRU YAFANYA KIKAO KUJADILI MRADI WA CRRI AWAMU YA PILI

Jumanne, 25 June 2024, Kibaha

Timu ya Menejimenti kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) wamefanya kikao cha warsha ya mradi wa “Coral Reef Rescue Initiative” wa awamu ya pili uliofanyika katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

Timu ya Menejimenti iliyoongozwa na Mratibu Mkuu wa Mradi Bw. Godfrey Ngupula walikutana na kufanya kikao hicho kwaajili ya kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu mradi ikiwemo kupitia mpango kazi na namna watakavyoenda kutekeleza malengo ya mradi huo kwa awamu hii ya pili.