KAIMU MENEJA MPRU ASHIRIKI HAFLA MAKABIDHIANO YA VIBANDA VYA UTALII KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA NA JAMII
KAIMU MENEJA MPRU ASHIRIKI HAFLA MAKABIDHIANO YA VIBANDA VYA UTALII KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA NA JAMII

Ijumaa, 22 Machi 2024, Tanga

Kaimu Meneja wa Hifadhi za Bahari za Meneo Tengefu Tanzania (MPRU), Bw. Davis Mpotwa ameshiriki katika hafla ya kukabidhi vibanda vya utalii pamoja na soko la samaki kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga na Jamii kupitia mwaliko wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WCS).

WCS imekuwa ikitekeleza mradi unaoitwa ‘Kuunda mtandao wa MPAs zinazostahimili uthabiti katika maeneo muhimu ya kimataifa ya Bahari ya Hindi Magharibi’ kwa kipindi cha miaka mitatu (2019-2023) unaolenga maeneo ya Pwani ya Kaskazini mwa Tanzania.

Kazi ya sasa ya WCS inalenga kuboresha ufanisi wa Usimamizi wa Maeneno ya Uhifadhi (MPAs) inayosimamiwa na serikali ambayo inachangia Uendelevu wa Ufanisi wa shughuli za Uhifadhi wa Bahari ndani ya Maeneo yaliyohifadhiwa Baharini.