UHIFADHI WA MATUMBAWE KATIKA BAHARI YA HINDI NI STAHIMILIVU KWA ASILIMIA 50
UHIFADHI WA MATUMBAWE KATIKA BAHARI YA HINDI NI STAHIMILIVU KWA ASILIMIA 50

Jumanne, Machi 25, 2026, Dar es Salaam

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. Godfrey Ngupula amesema Uhifadhi wa Matumbawe katika Bahari ya Hindi ni stahimilivu kwa asilimia hamsini (50) na kueleza kuwa elimu imekuwa ikitolewa kwa wakazi wanaoishi katika ukanda huo ili kuendeleza kuyatunza kutokana na asilimia zaidi ya sabini (70) ya jamii hiyo shughuli zao zinategemea matumbawe.

Mhifadhi Mkuu huyo aliyasema hayo Machi 24, 2026 katika Mkutano wa Tathmini ya Awamu ya tatu (3) wa Mradi wa Urejeshwaji wa Miamba ya Matumbawe (CRRI) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Tiffany Diamond iliyopo jijini Dar es Salaam.

“Sisi tumekuja kuhakikisha tunaongeza uelewa kwa watu lakini kuhakisha pia serikali na yenyewe inafanya kazi katika mazingira rahisi kwa kushirikisha watu wengi na jamii kubwa zaidi ili kuhakikisha hali inakaa vizuri” Alisema Bw. Ngupula.

Lakini namna gani tunaweza kusema kwamba kwa asilimia 50 bado ni stahimilivu tukijitahidi hapa tulipo ikaenda bora zaidi inakuwa ni jambo jema lakini isishuke zaidi ya hapa” Aliongezea Bw. Ngupula.

Naye kwa  upande wake, Mratibu wa Mipango ya Bahari kutoka Shirika la Uhifadhi Duniani (WWF) Dkt. Modesta Medard amewataka watekelezaji wa Mradi wa Uhifadhi kutekeleza kanuni zitakazo waongoza katika uoteshaji wa Matumbawe badala ya jamii kuja na hoja zake tofauti tofauti. 

“Tarehe moja mwezi wa nne lazima tuangalie kwamba tuje na guideline/muongozo utakaokuwa umetolewa na umehusisha jamii na wataalam ni jinsi gani Matumbawe yaweze kuwa restored kama tunavyofanya kwenye mangrove/mikoko kama tunavyofanya kwenye sea grass/ nyasi bahari basi na wao na hiyo guideline ama muongozo ambao sasa watakuwa wanauepeleka kwa jamii kwa kiswahili na kiingereza lakini huo muongozo pia lazima tuangalie nchi nyingine zinafanyaje” Alisema Dkt. Modest Bernard.