WADAU MBALIMBALI KUTOKA NCHI 30 WAKUTANA DSM KUMJADILI KASA
WADAU MBALIMBALI KUTOKA NCHI 30 WAKUTANA DSM KUMJADILI KASA

Jumanne, 25 June 2024, Dar es Salaam.

Wadau kutoka nchi mbalimbali takribani 30 zilizo kando ya Bahari ya Hindi ambazo zimesaini makubaliano ya uhifadhi wa Kasa wa baharini wamekutana kujadili na kupima hatua waliyofikia ya kuwalinda kasa hao tangu wasaini makubaliano. 

Hayo yamefahamika wakati Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe alipokuwa akifungua mkutano wa 9 wa nchi zilizoingia makubaliano ya kulinda Kasa na mazingira yake uliofanyika jijini Dar es Salaam Juni 24, 2024.

Prof. Shemdoe amesema wadau kutoka nchi hizo 30 wamekutana kuona wamefika wapi tangu waliposaini makubaliano ya kuwalinda Kasa ambao wapo kwenye hatari ya kutoweka duniani. 

Aidha, kwa upande wake Mhifadhi Mkuu kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. Godfrey Ngupula alieleza kuwa tayari washapokea ripoti za kila nchi, kanda pamoja na mapendekezo ikiwemo changamoto tayari kwaajili kufanya majadiliano mapana ili kuhakikisha kasa wanahifadhiwa.

Katika mkutano huo ambao unafanyika kwa siku nne kuanzia Juni 24 hadi 28, 2024, Tanzania ndio mwenyeji kupitia Kitengo cha Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) kilichopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.